NG-CDF YAELEZWA KUWA MKOMBOZI WA ELIMU VIJIJINI
Wakenya wametakiwa kuunga mkono mswada wa marekebisho ya Katiba unaolenga kuidhinisha rasmi Hazina ya Maendeleo ya Maeneobunge (NG-CDF) kuwa sehemu ya Katiba.
Wakazi wa eneobunge la Malindi, Kaunti ya Kilifi, wameeleza kuwa hazina hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa jamii, hasa kwa kuwasaidia wanafunzi wanaotoka katika familia maskini kupata elimu.
Aidha, wamesema kuwa fedha za NG-CDF zimechangia pakubwa katika kuboresha miundombinu ya shule mbalimbali, jambo ambalo limeimarisha mazingira ya ujifunzaji na kuongeza ufaulu miongoni mwa wanafunzi.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































