STARS WAANZA MATAYARISHO DHIDI YA MOROCCO
Timu ya Kenya Harambe Stars inajitayarisha kuchuana na Timu ya Morocco siku ya Alhamisi wiki hii katika mashindano ya CHAN 2024 baada ya kupata ushindi wa bao moja kwa bila hapo jana dhidi ya timu ya The Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye mechi yao ya ufunguzi ugani Kasarani jijini Nairobi.
Stars walioonekana kutawala mechi katika kipindi cha kwanza, walijipatia bao la ushindi kupitia kwa kiungo Austin Odhiambo katika dakika muda wa majeruhi ya kipindi cha kwanza, bao lililowahakikishia si unyakuzi wa pointi 3 pekee bali pia kila mmoja wa timu hiyo kupokea shilingi milioni 1 kama ilivyoahidiwa na Rais William Ruto.
Alhamisi hii stars wanatarajiwa kumenyana na Morocco ambao walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Angola katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, ushindi uliowapa alama 3 na uongozi kundi A wakifuatiwa na Kenya.
Kwingineko Tanzania waliwalaza Burkina Faso mabao 2-0 katika mechi yao ya ufunguzi wa mashindano hayo iliyochezwa Jumamosi nchini Tanzania.
Nao Madagascar walitoka sare ya kutofungana dhidi ya Mauritania.
Katika mechi za leo Niger watamenya na Guinea huku Uganda wakishuka diimbani kuchuana na Algeria
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































