KUNA UFADHILI WA KUTOSHA, OGAMBA
Ufadhili wa mikopo ya elimu ya juu HELB utatosha kuwafadhili wanafunzi wote wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vikuu mbali mbali mwezi ujao.
Haya ni kwa mujibu wa waziri wa elimu Julius Ogamba anayesema serikali itatenga fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anashughulikiwa ipasavyo.
Aidha amesema kuwa karo ya vyuo vikuu itapunguzwa huku akipuuzilia mbali madai kuwa hatua hiyo itasababisha hasara kwa vyuo vilivyo na madeni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































