BAJABER AREJEA KIKOSI CHA TAIFA
Mchezaji wa Simba, Mohammed Bajaber, ameahidi kurejesha imani aliyopewa baada ya kuitwa tena katika kikosi cha taifa cha Harambee Stars kufuatia kipindi kigumu alichopitia kutokana na majeraha.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka ishirini na mitatu amerejea kikosini kwa mara ya kwanza baada ya takriban mwaka mmoja, akisema kuwa kipindi hicho kilimjaribu sana kimwili na kiakili.
Bajaber amekiri kuwa mwaka uliopita ulikuwa miongoni mwa vipindi vigumu zaidi katika taaluma yake ya soka, lakini sasa ana azma ya kurejea kwa nguvu na kuonyesha uwezo wake uwanjani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































