AKONNOR AONYA GOR MAHIA BAADA YA KIPIGO CHA TUSKER
Kocha wa Gor Mahia Charles Akonnor amekiri kuwa makosa ya kizembe yaliigharimu timu yake katika kipigo cha 3-1 dhidi ya Tusker kwenye FKF Super Cup, huku akihofia makosa hayo yanaweza kuathiri safari yao ya kutwaa mataji msimu wa 2026/27.
Akonnor amesema mabao yote waliyofungwa yalitokana na makosa ya wachezaji binafsi, akisema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara na linahitaji kutatuliwa haraka kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
Gor Mahia, ambayo ni mabingwa wa Ligi Kuu ya FKF, ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi za wazi dhidi ya Tusker, hali iliyomlazimu Akonnor kuonya kikosi chake kuacha makosa ya kitoto iwapo wanataka kushindania mataji msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































