#Local News

RUTO AKOSOA UPINZANI, AAHIDI KUPUNGUZA BEI YA MBEGU

Rais William Ruto amewashambulia viongozi wa upinzani kwa kile alichosema ni kukosa sera na mipango ya wazi ya maendeleo, akidai badala yake wamejikita katika kuikosoa serikali bila kutoa suluhu kwa changamoto zinazowakabili Wakenya.

Akizungumza Kaunti ya Narok, Ruto amesema serikali yake inaendelea kutekeleza mipango ya kupunguza gharama za kilimo, akitangaza punguzo la shilingi 500 kwa gunia la mbolea ya ruzuku.

Rais pia ameahidi kupunguza kwa nusu bei ya mbegu za mahindi, hatua ambayo amesema inalenga kuwapa wakulima nafuu na kupunguza gharama ya pembejeo za kilimo nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *