POLISI KUVAA SARE MPYA KUANZIA WIKI IJAYO
Maafisa wa kawaida wa Huduma ya Polisi Kenya wataanza kuvaa sare mpya kuanzia wiki ijayo, baada ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi kutekeleza mapendekezo yaliyotokana na maoni ya umma kuhusu muonekano wa sare zao.
Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amesema maafisa wa polisi walipinga sare ya sasa ya rangi ya samawati iliyokolea wakati wa zoezi la ushirikishaji umma lililofanyika mwaka 2023, hatua iliyochangia kuanzishwa kwa mabadiliko hayo.
Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua rasmi sare hiyo mpya Ijumaa wakati wa hafla ya kuwaaga na kuwatunuku maafisa wapya wa polisi wanaomaliza mafunzo, kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa maafisa wa kawaida kote nchini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































