MURANG’A SEAL YAMWONGEZA LOPAGA KWENYE SAFU YA USHAMBULIAJI
Murang’a Seal imeongeza nguvu katika safu yake ya ushambuliaji baada ya kumsajili mshambuliaji Josphat Lopaga kutoka Kakamega Homeboyz, huku klabu hiyo ikilenga kufanya vizuri zaidi msimu wa 2026/27.
Lopaga anarejea katika klabu hiyo akiwa na jukumu la kusaidia Murang’a Seal kupanda kutoka nafasi ya nane iliyomaliza msimu uliopita, huku uzoefu wake katika ligi ya Kenya ukitarajiwa kuongeza makali mbele ya lango.
Mshambuliaji huyo amewahi kuchezea Mt Kenya United, Posta Rangers na AFC Leopards, kabla ya kuhamia nje ya nchi ambako aliwahi kuitumikia Dhofar ya Oman pamoja na Dinamo Brest na Naftan Novopolotsk ya Belarus kwa mkopo, hivyo kuleta uzoefu mpana katika kikosi cha Murang’a Seal.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































