#Football #Sports

BRUNO FERNANDES ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA ENGLAND

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes ametawazwa mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa PFA, baada ya msimu wa 2025/26 uliomweka kileleni mwa rekodi za Ligi Kuu Uingereza.

Fernandes aliweka rekodi mpya ya pasi 21 za mabao katika msimu mmoja wa Ligi Kuu, akivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Thierry Henry na Kevin De Bruyne, huku pia akifunga mabao tisa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alisaidia Manchester United kurejea katika nafasi ya tatu baada ya mwanzo mbaya wa msimu, na hivyo kufuzu tena kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku tuzo ya wanawake ikienda kwa Khadija Shaw wa Manchester City kwa mara ya pili.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *