#Local News

LAGAT AWAONYA WAHUSIKA WA VURUGU KWENYE SIASA

Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi, DIG Eliud Lagat, amezungumzia ongezeko la vurugu na uhuni unaohusishwa na shughuli za kisiasa nchini.

Lagat amesema vyombo vya usalama vina wajibu wa kuhakikisha mikutano na shughuli za kisiasa zinafanyika kwa amani, huku wakichukua hatua dhidi ya watu wanaotumia vurugu kuvuruga utulivu.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba wahusika wa vurugu na uhuni watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *