#Local News

WASHUKIWA WATATU WA TUKIO LA KIATU DHIDI YA RUTO WAACHILIWA BILA MASHITAKA

Watu watatu waliokamatwa kwa kudaiwa kumtupia kiatu Rais William Ruto wakati wa hafla ya umma huko Migori, wameachiwa bila mashitaka baada ya uchunguzi kubaini kuwa kitendo hicho hakikuwa cha makusudi.

Tukio hilo lilitokea Mei 5, wakati wa ziara ya rais ya kikazi ya siku tatu kaunti ya Migori.

Maafisa wa usalama walichukua hatua haraka na kuwakamata watu watatu walioshukiwa kuwa walihusika huku wachunguzi wakibaini kuwa hakukuwa na nia wazi ya kumlenga Rais.

Imetayarishwa na Janice Marete

WASHUKIWA WATATU WA TUKIO LA KIATU DHIDI YA RUTO WAACHILIWA BILA MASHITAKA

MWANGA WA TUMAINI NGARA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *