KRU KUPANGA UPYA MUUNDO WA KENYA CUP ILI KUREJESHA USHINDANI
Muungano wa Raga Kenya (KRU) unapanga kufanya marekebisho makubwa ya mashindano
ya Kenya Cup katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, hatua inayolenga kurejesha ushindani
na kuvutia wadhamini zaidi wa kibiashara.
Chini ya pendekezo jipya, ligi itagawanywa katika viwango viwili. Kiwango cha Kwanza
(Tier One) kitakuwa na klabu sita bora, huku Kiwango cha Pili (Tier Two) kikijumuisha
klabu sita za mwisho kwenye msimamo wa ligi.
Mfumo wa kupandishwa na kushushwa daraja utatekelezwa kikamilifu, ambapo timu mbili
za mwisho katika Tier One zitashushwa hadi Tier Two, na timu mbili bora kutoka Tier Two
zitapandishwa daraja.
Mapendekezo hayo yanakuja kufuatia matokeo mabaya yasiyo na uwiano yaliyojitokeza
mwanzoni mwa msimu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































