CITY WATIWA BREKI EPL
Azma ya Manchester City kupelekana sako kwa bako na Arsenal kwenye kinyang’anyiro cha kuwania ligi kuu ya soka nchini Uingereza EPL ilitiwa doa jana usiku, baada ya vijana hao wa Pep Guardiola kushikwa kwenye sare ya kutofungana dhidi ya Sunderland.
Mawimbi ya mashambulizi ya City yalionyeshwa giza ugani Stadium of Light, na kutamatisha rekodi yao ya kushinda mechi 8 mfululizo iliyoibua ushindani mkali na Arsenal.
Hata hivyo, City wanaifuata Arsenal kwa pointi 4 baada ya nusu ya msimu, na watahitaji kujiimarisha ili kuendeleza ushindani dhidi ya Arsenal ambayo inaendelea kuvuna ushindi hata katika mechi zinazoonekana ngumu.
Katika matokeo mengine, Liverpool walishikwa kwenye sare ya kutofungana na Leeds United.
Jumla ya sare 4 zilishuhudiwa katika mechi zote za jana, Tottenham wakishikwa na Brentford huku Crystal Palace na Fulham wakitoa sare ya goli moja.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































