UPINZANI WASISITIZA UMOJA, KUMTANGAZA NAHODHA
Muungano wa upinzani umesema kwamba uko katika hatua za mwisho za kumtangaza mgombea wake wa urais atakayemenyana na Rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao, na utamweka wazi baada ya kongamano la kitaifa la wajumbe, NDC, la chama cha DCP chake aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua.
Wakizungumza baada ya NDC ya chama cha DP chake Justin Muturi, viongozi wa muungano huo wamesema watafanya kila wawezalo kusalia Pamoja ili kujiimarisha kwenye uchaguzi huo.
Miongoni mwa wawaniaji hao ni Fred Matiang’i, Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua, Eugene Wamalwa, Justin Muturi na Martha Karua.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































