WANG’AYA AJIUNGA NA NAIROBI UNITED
Kiungo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Kevin Wang’aya, amejiunga na klabu ya Nairobi United akilenga kusaidia timu hiyo kufanya vyema na kupigania nafasi za juu msimu huu.
Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwake, Wang’aya amesema yuko tayari kwa changamoto mpya, akiahidi kuleta ubunifu, nguvu na udhibiti katika safu ya kiungo ili kusaidia timu kufikia malengo yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anajiunga na Nairobi United akiwa na wasifu mzuri, baada ya kung’ara na Rising Stars na kusaidia Kenya kufuzu kwa Kombe la Afrika la vijana wa chini ya miaka 20 kwa mara ya kwanza, hatua iliyomuingiza pia katika kikosi bora cha hatua ya makundi ya mashindano hayo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































