#Business

UJENZI WA TALANTA STADIUM KUGHARIMU BILIONI 10 ZAIDI YA BAJETI- RIPOTI

Gharama ya ujenzi wa uwanja wa Talanta jijini Nairobi wenye uwezo wa kuwabeba watu 60,000 imeongezwa kwa Ksh10.85 bilioni, kulingana  na Mkaguzi Mkuu wa serikali Nancy Gathungu.

Katika ripoti mpya ya ukaguzi wa hesabu za Wizara ya Ulinzi ya 2024/25, Gathungu anahoji tofauti ya bei isiyoelezeka katika mradi huo, akibainisha kuwa Hazina ya Kitaifa iliidhinisha Ksh35 bilioni kutoka kwa Hazina ya Maendeleo ya Jamii ya Michezo na Sanaa (SASDF) chini ya mpango wa malipo wa miaka sita.

Hata hivyo, kandarasi hiyo ilitiwa saini kwa Ksh45.85 bilioni, na kusababisha tofauti isiyoeleweka ya Ksh10.85 bilioni zaidi.Kufuatia ripoti, ni kwamba kibali kutoka kwa Mwanasheria Mkuu wa wakati huo Justin Muturi hakikupatikana, kinyume na sheria ya ununuzi inayohitaji idhini ya mwanasheria kwa kandarasi ya zaidi ya Ksh5 bilioni.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

UJENZI WA TALANTA STADIUM KUGHARIMU BILIONI 10 ZAIDI YA BAJETI- RIPOTI

SHA KUGHARAMIA UZAZI LEVEL 2 NA 3-

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *