SHUJAA WAJIPANGA MASHINDANO BRAZIL
Timu za taifa za raga ya wachezaji saba kwa upande wa wanaume na wanawake zinajiandaa kwa wikendi muhimu nchini Brazil, ambapo hatua ya mwisho ya mashindano ya daraja la pili itafanyika São Paulo kuanzia Machi 28 hadi 29
Kwa matumaini ya kupanda daraja, Shujaa na Kenya Lionesses wanaingia mashindano wakiwa na kila sababu ya kupigania ushindi, huku Shujaa wakifika wakiwa na ari baada ya kushinda medali ya shaba mjini Montevideo walipoishinda Uruguay 22-14. Matokeo hayo yaliwaweka nafasi ya tatu kwa alama 32, wakikaribia nafasi mbili za juu.
Kampeni ya Shujaa itaanza Jumamosi kwa mechi tatu mfululizo, wakianza dhidi ya Ujerumani saa kumi na dakika ishirini na mbili jioni, kisha Ubelgiji saa moja na dakika kumina mbili usiku, na kumalizia dhidi ya Canada saa nne na dakika ishirini na moja usiku.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































