MATARAJIO YA WAFANYAKAZI LEBA DEI
Huku Kenya ikijiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya wafanyakazi, Leba dei, wafanyakazi nchini wanatarajia tangazo la nyongeza ya mishahara kwa asilimia 23 kutokana na ongezeko la gharama ya maisha.
Katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, COTU, Francis Atwoli, amesema kuwa maafisa wakuu serikalini, wawakilishi wa mashirika na vyama mbali mbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za leo zinazoandaliwa katika kaunti ya Vihiga.
Waziri wa Leba Alfred Mutua, amedokeza uwezekano wa Rais William Ruto kutangaza afueni kwa wafanyakazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































