#Local News

EACC YAIDHNISHWA KUTWAA MALI YA AFISA WA ZAMANI NAIROBI JIMMY KIAMBA

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imeanzisha mchakato wa kutwaa mali na pesa za aliyekuwa afisa mkuu wa fedha katika kaunti ya Nairobi Jimmy Kiamba baada ya jopo la majaji watano wa mahakama ya rufaa kudumisha uamuzi wa mahakama kuu ambapo Kiamba alikuwa amepinga mchakato huo.

Katika uamuzi huo, majaji hao wamekubaliana na EACC kwamba afisa huyo wa zamani anamiliki mali na pesa asizoweza kueleza chanxo chake.

Kwa mujibu wa EACC, serikali inalenga kutwaa shilingi milioni 113 zilizoko katika akaunti mbali mbali za benki na majumba saba ya kifahari.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *