“MBEBA MAONO NI MIMI!” LUSAKA ASEMA KWENYE MAGEUZI
Gavana wa kaunti ya Bungoma Ken Lusaka amefanya mageuzi katika baraza lake la mawaziri na kuwateua maafisa wakuu wapya katika wizara mbali mbali katika kile alichosema kuimarisha utendakazi
Miongoni mwa wlaioathirika ni Hebert Kibunguchi ambaye amehamishwa kutoka idara yam aji hadi idara ya elimu na kuchukua mahali pa David Wamamili ambaye amehamishiwa idara ya biashara.
Carolyne Khalayi amehamishwa kutoka idara ya Biashara hadi idara ya afya, na kuchukua mahali pa Andrew Wekesa ambaye amehamishiwa idara ya maji na mali asili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































