JOHO AMJIBU GACHAGUA KUHUSU MADAI YA KURA KUIBWA
Waziri wa Madini na Uchumi wa Buluu Hassan Joho amepuuzilia mbali madai ya kuwepo kwa mpango wa kuiba kura katika uchaguzi wa 2027, akimtaka kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kuacha kumlenga Naibu Mwenyekiti wa IEBC Fahima Araphat Abdallah.
Joho amesema hakuna mpango wowote wa kuhujumu uchaguzi, huku akimtaka Gachagua kutomchagua Fahima kama mlengwa wa shutuma hizo, akisisitiza kuwa huenda analengwa kwa sababu anatoka katika jamii ya wachache.
Kauli hiyo inajiri baada ya Gachagua kudai kuwa kuna njama ya kuathiri uchaguzi wa 2027 kupitia mfumo mpya wa teknolojia ya uchaguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































