#Athletics #Sports

WANYONYI AONGOZA NYOTA WA KENYA ZURICH

Wanariadha wa Kenya Emmanuel Wanyonyi, Julius Yego, Timothy Cheruiyot, Phanuel Koech na Faith Cherotich nchi katika mashindano ya Diamond League jijini Zurich hii leo.

Wanyonyi anaingia kwenye mashindano hayo akiwa na motisha baada ya kutwaa ushindi wake wa kwanza wa Diamond League msimu huu mjini Lausanne mwishoni mwa wiki, akishinda mbio za mita 800 kwa muda wa dakika 1:42.19.

Bingwa huyo wa Olimpiki na dunia wa mita 800 sasa analenga kuendeleza mfululizo wa ushindi, huku akijiandaa kwa Fainali za Diamond League mjini Brussels na Mashindano ya Dunia ya Ultimate yatakayofanyika Budapest, Hungary.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *