#Local News

KENYA YAADHIMISHA MIAKA 16 YA KATIBA YA 2010

Kenya leo inaadhimisha Siku ya Katiba, miaka 16 tangu kupitishwa kwa Katiba ya mwaka 2010, siku ambayo inalenga kuwakumbusha Wakenya kuhusu haki, wajibu na misingi ya utawala wa kikatiba.

Rais William Ruto alitangaza tarehe 27 Agosti kuwa Siku ya Katiba ili kuadhimisha kutangazwa rasmi kwa Katiba ya 2010, huku siku hiyo ikiwa ni ya kazi badala ya likizo ya kitaifa.

Rais Ruto anatarajiwa kuongoza sherehe za kitaifa za kuadhimisha miaka 16 ya Katiba, huku Wakenya wakitakiwa kuendelea kuthamini na kulinda misingi ya Katiba pamoja na haki na uhuru unaotambuliwa kisheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *