#Sports #Volleyball

MALKIA STRIKERS YALENGA USHINDI DHIDI YA MALI

Kocha wa Malkia Strikers Geoffrey Omondi anataka timu hiyo kujenga juu ya ushindi wao mkubwa dhidi ya Zambia watakapokutana na Mali hii leo katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A kwenye Mashindano ya Afrika ya Mpira wa Wavu ya Wanawake katika Uwanja wa Ndani wa Kasarani.

Kenya ilianza kampeni yake ya kutetea taji kwa kishindo Jumanne usiku baada ya kuifunga Zambia seti 3-0, kwa alama 25-14, 25-9 na 25-11, huku Omondi akipata nafasi ya kuwachezesha wachezaji mbalimbali.

Omondi amesema siku ya mapumziko hapo jana ilitumiwa kuwawezesha wachezaji kupata nafuu na kujiandaa kwa Mali, kabla ya mashindano kuingia katika hatua ya mtoano, huku timu hiyo ikilenga kuendeleza kiwango chake kizuri.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *