#Football #Sports

MBAPPÉ AFUNGA HAT-TRICK REAL MADRID IKIICHAPA REAL SOCIEDAD

Kylian Mbappé alifunga mabao matatu na kuisaidia Real Madrid kuichapa Real Sociedad 4-1 katika Ligi Kuu ya Uhispania, katika mchezo wa kwanza wa nyumbani wa kocha José Mourinho tangu arejee Santiago Bernabéu.

Madrid imeendeleza mwanzo wake mzuri kwa kupata ushindi wa pili mfululizo, huku Vinícius Júnior pia akifunga na Jude Bellingham akitoa pasi mbili za mabao, katika mchezo ambao safu hiyo ya nyota iliisumbua Sociedad.

Mourinho aliendelea na kikosi kilichomsaidia Madrid kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Espanyol mwishoni mwa wiki, katika mchezo wake wa kwanza tangu kurejea kuinoa klabu hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus SIfuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *