#Football #Sports

APS BOMET YALENGA KUMALIZA TANO BORA MSIMU MPYA

APS Bomet imebadilisha mtazamo wake kutoka kupigania kusalia ligi kuu hadi kulenga mafanikio makubwa, huku ikijiandaa kwa msimu wa SportPesa League 2026/27

Kocha mkuu Sammy “Pamzo” Omollo amesema tofauti na msimu uliopita ambapo alipewa jukumu la kuinusuru timu isishuke daraja, safari hii wanalenga kumaliza katika nafasi tano bora mwishoni mwa msimu

APS Bomet ilimaliza nafasi ya kumi katika msimu wake wa kwanza ligi kuu, huku sehemu kubwa ya kikosi ikibaki, na Omollo anaamini mwendelezo wa kikosi, uimara wa ulinzi na kujiamini zaidi kutawasaidia kushindana kwa nafasi za juu msimu huu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *