#Local News

HATIMAYE MASHINE YA KUUNDA CHAPATI  ZA WANAFUNZI JIJINI NAIROBI YAWASILI NCHINI

Mpango wa lishe shuleni wa Dishi na County jijini Nairobi umeongeza chapati katika menyu yake baada ya kuwasili na kusakinishwa kwa mashine iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Mashine hiyo imewekwa  katika Jiko la  shule ya musingi ya Toi  eneo la Kibera, aidha mashine hiyo imeripotiwa kuwa na  uwezo wa kutengeneza chapati 2,000 kwa saa.

Kwa mujibu wa taarifa ni kuwa Chapati hizo zitasambazwa kwa shule kwa ratiba maalum inayolingana na kalenda ya mpango wa lishe na  kuwawezesha wanafunzi katika shule mbalimbali za kaunti kupata chapati katika siku zilizopangwa.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *