#Local News

VIJANA WARAIWA KUJITENGA NA UHUNI

Baraza la Wazee wa Kalenjin limewataka vijana nchini kukataa kutumiwa na wanasiasa kuzua vurugu, huku Uchaguzi Mkuu wa 2027 ukikaribia.

Wakizungumza mjini Eldoret, wazee hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Myoot Council of Elders Benjamin Kitur, wamewataka wanasiasa na wafuasi wao kudumisha amani na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.

Wamesema viongozi wanapaswa kuruhusiwa kuwasilisha sera na mipango yao kwa wananchi, ambao watakuwa na fursa ya kufanya uamuzi wao kupitia kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *