#Local News

WAKULIMA TRANS NZOIA WATAKA BEI YA MBOLEA KUFIKA SHILINGI 1,500

Wakulima katika Kaunti ya Trans Nzoia wamekaribisha hatua ya serikali kupunguza bei ya mbolea, wakisema itawapunguzia gharama za uzalishaji.

Hata hivyo, wakulima hao wameitaka serikali kufanya punguzo zaidi ili bei ya mfuko wa mbolea ishuke hadi shilingi 1,500.

Wamesema bei nafuu ya mbolea itawasaidia kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji wa chakula, huku wakiitaka serikali kuendelea kuweka mikakati ya kuwasaidia wakulima kukabiliana na gharama za uzalishaji.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

WAKULIMA TRANS NZOIA WATAKA BEI YA MBOLEA KUFIKA SHILINGI 1,500

VIJANA WARAIWA KUJITENGA NA UHUNI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *