AFCON KUFANYIWA MAGEUZI, CAF
Soka la bara Afrika imeratibiwa kufanyiwa marekebisho makubwa, ikiwemo kubuniwa kwa dimba la African Nations League na kubadilishwa kwa dimba la AFCON ambalo litakuwa likiandaliwa kila baada ya miaka 4 tofauti na miaka 2 ya sasa.
Katika taarifa kwa wanahabari baada ya mkutano na wadau, Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF Dakta Patrice Motsepe, amesema AFCON ya mwaka 2027 itakayoandaliwa na Kenya, Uganda na Tanzania itafanyika jinsi ilivyopangwa, ila ile ya mwaka wa 2029 itaandaliwa mwaka wa 2028 ili kupisha mageuzi mapya AFCON inayofuata ikiandaliwa mwaka 2032.
Mabadiliko hayo yatapisha kufanyika kwa African Nations League ya kwanza mwaka wa 2029, ambayo Motsepe anasema itajumuisha mataifa yote 54.
Hata hivyo, uongozi wa CAF haukuweka wazi mara moja iwapo Ligi hiyo itakuwa ya kila mwaka au baada ya miaka 2.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































