OGAMBA AONYA DHIDI YA SIASA SHULENI
Waziri wa Elimu Julius Ogamba amewaonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kuingiza siasa katika masuala ya elimu, akisema hulka hizo zinaibua hofu miongoni mwa wazazi na wanafunzi nchini.
Akizungumza katika kaunti ya Murang’a, Ogamba amerejelea kauli ya aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua kwamba wanafunzi wajiunge na shule za kitaifa zilizo katika maeneo wanakotoka, akisisitiza kuwa lengo la shule za kitaifa ni kuwahudumia wanafunzi kutoka maeneo yote ya taifa.
Amekariri haja ya shule hizo kutoa nafasi sawa kwa wanafunzi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































