WAWEKEZAJI WA CHINA WAVUTIWA NA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA MBALI MBALI KENYA
Kundi la wawekezaji kutoka China liko nchini Kenya kutafiti fursa za uwekezaji katika sekta za miundombinu na kilimo nchini. Mwanzilishi na mwenyekiti wa kundi la ushawishi wa biashara la China, Fortune Generation, Martin Hang amesema wawekezaji wa China wanachukua nafasi muhimu katika kuboresha miundombinu na katika sekta ya usalama wa chakula nchini Kenya. Hang aidha amesema wawekezaji wa China wana uwezo wa teknolojia na fedha kujenga barabara za kisasa, bandari, na viwanda vya kuzalisha nishati.
Kwa upande wake kaimu meneja wa uwekezaji na mawasiliano ya mashirika katika Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji Bidhaa Nje, Moses Kipkebut amesema, Kenya inatafuta kufaidika kutokana na uzoefu wa China katika kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo. Kipkebut vile vile ameongeza kuwa, Kenya imeandaa kanuni rafiki za ushuru katika maeneo ya uzalishaji bidhaa nje ili kuwawezesha wawekezaji wa kigeni kusaidia kuibadili nchi hii kuwa kituo cha kikanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































