VIKWAZO KWA IEBC KUBUNI MAENEO MAPYA
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC haitafanikiwa kuangazia upya mipaka ya maeneo bunge na wadi kabla ya uchaguzi mkuu ujao, na badala yake itafanya zoezi hilo kwa awamu kutokana na changamoto za kikatiba, kiutendaji na kisheria.
Kwenye kikao na wanahabari, mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon, amesema vikwazo hivyo vimesababishwa na sababu kadhaa ikiwemo kukosekana kwa makamishna afisini kwa muda mrefu na kesi zinazoendelea mahakamani kuhusu uhalali wa hesabu ya watu yaani sensa ya mwaka 2019 katika baadhi ya maeneo.
Aidha, amesema zoezi la usajili wa wapiga kura katika kiwango cha wadi litaanza mwezi Machi mwaka huu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































