#Local News

FAMILIA YAPOTEZA WATU SITA KWA AJALI YA MALAHA

Familia moja kutoka Wadi ya Mihuu katika Eneo Bunge la Webuye Mashariki inaomboleza vifo vya watu sita wa familia hiyo waliofariki katika ajali ya barabarani iliyotokea Malaha Junction kwenye barabara ya Webuye–Kitale, ajali iliyosababisha vifo vya watu 15.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo Ezekiel Kinisu, jamaa hao walikuwa wamekusanyika eneo hilo kushuhudia ajali ya awali iliyohusisha waendesha bodaboda kabla ya lori lililokuwa likitoka upande wa Kitale kupoteza mwelekeo na kuwagonga watu waliokuwa kando ya barabara.

Manusura kadhaa wanaendelea kupokea matibabu katika Hospitali ya Kaunti ya Webuye, huku daktari msimamizi David Wanikina akisema juhudi zote zinafanywa kuwaokoa waliojeruhiwa vibaya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *