SAKAJA: WAFANYABIASHARA WA GIKOMBA SHARTI WAHAME
Serikali ya kaunti ya Nairobi imekariri kuwa wafanyabiashara wote walio ndani ya umbali wa mita 50 kutoka Mto Nairobi katika soko la Gikomba ni sharti wahame licha ya pingamizi hapo jana, ikisema wametengewa sehemu mbadala sokoni humo kwa muda ujenzi wa soko jipya unapoendelea.
Zoezi la kutathmini umbali huo hapo jana lilisitishwa ghafla baada ya wafanyabiashara hao kuzua rabsha, kwa misingi kwamba walikubaliana umbali wa mita 30 na wala si 50.
Kulingana na gavana Johnson Sakaja, hatua ya mazungumzo imepita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































