LISHE HATARI YAWAUA 4 KITUI
Polisi katika eneo la Kyuso kaunti ya Kitui wanachunguza kisa ambapo watu 4 kutoka Kijiji cha Nganda wamefariki baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa kibovu.
Akithibitisha vifo hivyo, OCPD wa Kyuso Edwin Otieno, amesema waathiriwa walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wamekutana nyumbani wka mkazi mmoja eneo hilo ambako walishiriki chakula cha Pamoja, na kisha wakaanza kulalamikia maumivu ya tumbo.
Kulingana na Otieno, watu watatu walifariki wakiwa njiani kuelekea katika hospitali Kyuso level 4, wa nne akafariki alipokuwa akipokea matibabu na wengine watatu wanaendelea kutibiwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































