WANJIGI; SERIKALI INANIULIZA NINI?
Serikali ya rais william Ruto ikona nia ya kuniangamiza, haya ni kwa mujibu wa mfanyibiashara Jimmy Wanjigi kufuatia uvamizi wa nyumba yake eneo la Muthaiga wiki jana.
Wanjigi anadai kuwa sio mara ya kwanza kwa maafisa wa usalama kutatiza amani katika makazi yake kwani kulingana naye hata wakati wa utawala wa rais mstaafu uhuru Kenyatta bado makazi yake yalivamiwa na maafisa wa polisi.
Wanjigi aidha ameibua madai kwamba rais mstaafu uhuru kenyatta na rais WilliAM Ruto wana njama fiche dhidi yake akiwataka kuweza wazi wanachokitaka kutoka kwake.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































