PAC YAMTAKA PS OLOLTUA KUELEZA KUSITISHWA KWA NEMIS
Kamati ya Hesabu za Umma imemtaka Katibu Mkuu wa Elimu ya Msingi John Ololtua kueleza sababu zilizofanya serikali kuachana na mfumo wa NEMIS katika usambazaji wa fedha kwa taasisi za elimu.
Kamati hiyo imehoji pia tofauti katika mgao wa fedha za ruzuku kwa shule zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, ikitaka maelezo kuhusu namna fedha hizo zilivyogawiwa.
PAC imeonya kuwa udhaifu katika mifumo ya usimamizi wa taarifa unaweza kuhatarisha matumizi sahihi ya fedha za umma, na kuitaka Wizara ya Elimu kuweka wazi hatua zinazochukuliwa kuhakikisha ruzuku inawafikia walengwa kwa usahihi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































