WANYONYI ASHINDA ZURICH NA KUWEKA REKODI BORA DUNIANI
Mkenya Emmanuel Wanyonyi amepata ushindi wake wa pili mfululizo katika mbio za mita 800 za Diamond League baada ya kumshinda Mualgeria Djamel Sedjati katika mashindano ya Zurich
Wanyonyi alionekana kupoteza nguvu akiwa amebakiza mita 100, jambo lililompa Sedjati nafasi ya kumkaribia, lakini Mkenya huyo alishikilia kasi hadi mstari wa mwisho na kushinda kwa dakika 1:41.76, muda bora zaidi duniani msimu huu
Ushindi huo umeboresha muda wake wa 1:42.19 alioweka wiki iliyopita Silesia, huku Wanyonyi sasa akielekeza nguvu zake katika fainali za Diamond League mjini Brussels, ambako atalenga kutetea taji lake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































