#Football #Sports

CHELSEA KUMSAJILI EMILIANO MARTÍNEZ KWA £7.5 MIL

Chelsea imefikia makubaliano na Aston Villa kumsajili mlinda lango wa Argentina Emiliano Martínez kwa ada ya pauni milioni 7.5, huku mchezaji huyo tayari akitoa idhini ya kuhamia Stamford Bridge.

Martínez mwenye umri wa miaka 33 anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili wenye chaguo la kuongeza mwaka mmoja, huku uhamisho huo ukitarajiwa kuipa Chelsea uzoefu zaidi katika nafasi ya kipa baada ya kiwango kisichoridhisha cha Robert Sánchez mwanzoni mwa msimu.

Uhamisho huo unamrejesha Martínez katika ushindani wa Ligi Kuu England akiwa ameichezea Aston Villa kwa miaka sita, baada ya kujiunga nayo akitokea Arsenal mwaka 2020.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *