RUTO AKIRI MAKOSA KATIKA KUSHUGHULIKIA MAANDAMANO
Rais William Ruto amekiri kuwa serikali yake ilifanya makosa katika namna ilivyoshughulikia maandamano ya 2024 na maandamano ya kuadhimisha kumbukumbu zake mwaka 2025, akisema hakuna damu iliyopaswa kumwagika wakati wa maandamano hayo.
Ruto sasa ameelekeza uchunguzi kuhusu vifo, madai ya utekaji nyara na matumizi ya nguvu kupita kiasi yaliyotokea wakati wa maandamano hayo, akisisitiza umuhimu wa kubaini ukweli kuhusu yaliyotokea.
Rais amesema uchunguzi wa kuaminika ndio njia pekee ya kubaini ukweli na kuhakikisha haki inatendeka, huku akisisitiza kuwa madai ya ukiukaji wa haki yanapaswa kuchunguzwa kikamilifu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































