#Local News

KANJAMA AIBUA WASIWASI KUHUSU UWAJIBIKAJI MAHAKAMANI

Rais wa Chama cha Wanasheria nchini Charles Kanjama, ameeleza wasiwasi kuhusu udhaifu unaodaiwa kuwepo katika mfumo wa mahakama, akisema baadhi ya michakato ya uwajibikaji inaweza kuzuiwa huku rufaa zikikabiliwa na vikwazo vya kiutaratibu vinavyochelewesha kesi.

Kanjama amesema hali hiyo imeangaziwa zaidi kufuatia mgomo wa kitaifa wa mawakili dhidi ya baadhi ya maafisa wa mahakama, ambao ulizua mjadala kuhusu uwajibikaji ndani ya Idara ya Mahakama.

Kanjama ametaja pia visa ambapo mahakama zilisitisha uchunguzi wa awali wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi EACC dhidi ya majaji au maafisa wa mahakama, akisema hali hiyo inazua maswali kuhusu namna uwajibikaji unavyotekelezwa ndani ya mahakama.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *