WABUNGE WATAKA UFAFANUZI KUHUSU UMILIKI WA eCITIZEN
Wabunge wameitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu umiliki wa mfumo wa eCitizen, wakati Hazina ya Kitaifa ikipanga kuweka usimamizi wa mfumo huo chini ya kanuni mpya.
Kamati ya Bunge ya Sheria Zilizokabidhiwa, iliyoongozwa na Mbunge wa Ainabkoi Samuel Chepkonga, imehoji suala hilo ilipokuwa ikichunguza kanuni zinazopendekezwa za Usimamizi wa Mfumo wa eCitizen za mwaka 2026.
Kanuni hizo zinapendekeza kuweka umiliki, udhibiti, uhifadhi wa mfumo, usimamizi na matengenezo ya eCitizen chini ya Hazina ya Kitaifa, hatua ambayo imeibua maswali kutoka kwa wabunge kuhusu nani hasa anamiliki mfumo huo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































