WAUGUZI KISUMU NA KAKAMEGA WAGOMA KUSITISHA MGOMO
Wauguzi katika kaunti za Kisumu na Kakamega wameapa kuendelea na mgomo wao hadi matakwa yao yatakapotimizwa, wakisisitiza kuwa hawako tayari kurejea kazini bila suluhu ya kudumu
Wahudumu hao wa afya wamesema wakati wa mazungumzo umepita, na sasa serikali za kaunti zinapaswa kukubaliana na matakwa yao na kukutana nao mezani kama washirika wenye usawa
Wamesisitiza kuwa mgomo huo utaendelea hadi pande zote zitakapofikia makubaliano yanayoshughulikia kikamilifu malalamishi na matakwa ya wauguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































