#Football #Sports

TIMU YA CAF YAKAGUA MAANDALIZI YA AFCON 2027 NCHINI KENYA

Timu ya ukaguzi wa kiufundi kutoka Shirikisho la Soka Afrika CAF imewasili Nairobi kukagua maandalizi ya Kenya kuelekea mashindano ya AFCON 2027, yatakayoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amepokea ujumbe huo unaoongozwa na Mkuu wa Mashindano wa CAF Khaled Nassar, akisema Kenya imejitolea kutimiza mahitaji yote ya CAF na kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa mafanikio.

Ukaguzi huo unafanyika baada ya mikutano ya uangalizi ya PAMOJA, ambapo mataifa hayo matatu yalithibitisha dhamira yao ya kuandaa mashindano bora yatakayoiweka Afrika Mashariki katika nafasi muhimu ya michezo na utalii barani Afrika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *