KRA YAKANA MADAI YA KUONGEZA USHURU
Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini, KRA, imesema haijaongeza ushuru wa biashara, bali inatekeleza tu viwango vya ushuru vilivyoidhinishwa na Bunge.
Kamishna wa Forodha wa KRA, Lilian Nyawanda, amesema hayo akijibu malalamiko ya wafanyabiashara hapa jijini Nairobi. Wafanyabiashara wamekuwa wakilalamikia ongezeko la gharama za kufanya biashara.
Nyawanda amesema KRA haina mamlaka ya kuongeza ushuru bila idhini ya Bunge, na kwamba inatekeleza sheria na viwango vya ushuru vilivyopitishwa na wabunge.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































