MUSALIA MUDAVADI KUMWAKILISHA RAIS RUTO LUANDA ANGOLA
Waziri Mkuu wa Serikali na Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi anatarajiwa kuelekea Luanda nchini Angola, ambako atamwakilisha Rais William Ruto katika mkutano wa Umoja wa Afrika, AU, utakaofanyika Agosti 30 mwaka huu.
Mkutano huo utajadili namna ya kuzuia na kumaliza migogoro inayotokea katika nchi mbalimbali za Afrika.
Safari ya Mudavadi inakuja wakati Kenya ikiendelea kushiriki katika juhudi za Umoja wa Afrika za kutafuta amani na kusaidia nchi za Afrika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































