#Local News

KENYA AIRWAYS YAPOTEZA SHILINGI MILIONI 905 KWA MGOMO

Shirika la Ndege la Kenya Airways limesema limepoteza zaidi ya dola milioni saba, sawa na zaidi ya shilingi milioni 904 kutokana na mgomo wa siku tatu uliovuruga shughuli za usafiri wa anga.

KQ imesema hasara hiyo inajumuisha mapato yaliyopotea pamoja na gharama za malazi, chakula, usafiri na kuwahamisha abiria kwenye safari nyingine.

Wakati wa mgomo huo, ndege 63 zilifutwa na zaidi ya safari 160 kuchelewa kwa wastani wa zaidi ya saa sita, huku zaidi ya tani 370 za mazao na nyama zikishindwa kusafirishwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *