ASKARI MKUU WA MAGEREZA APATIKANA AMEFARIKI RUIRU
Afisa mkuu wa Huduma ya Magereza amepatikana amefariki ndani ya gari katika eneo Spur Mall, Ruiru, Kaunti ya Kiambu, huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu kifo chake cha ghafla
Marehemu ametambuliwa kuwa Eric Kiarie Wainaina mwenye umri wa miaka 40, alikua akihudumu katika Makao Makuu ya Kanda ya Kati mjini Nyeri
Polisi wa Kituo cha Mugutha wamesema mwananchi alitoa taarifa baada ya kumwona afisa huyo ndani ya gari aina ya Nissan Wingroad, kabla ya maafisa kufika eneo hilo na kuthibitisha kisa hicho.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































