MASENETA WAWAKOSOA MAGAVANA KWA MGOMO WA WAUGUZI
Maseneta wamekosoa Baraza la Magavana kwa kuchelewesha kutatua mzozo wa wauguzi ambao umeathiri huduma muhimu za afya katika hospitali nchini kwa zaidi ya siku 40.
Wakizungumza Seneti baada ya kurejea kutoka mapumzikoni, maseneta wamesema serikali za kaunti zilipewa fedha za kutosha kushughulikia maslahi ya wahudumu wa afya, wakisema kutotatua mgomo huo kunaweza kuzidisha hali ya sekta hiyo.
Wabunge hao pia wametaka kuangaliwa upya kwa wazo la kuanzishwa kwa Tume ya Afya, huku madaktari wakitishia kujiunga na mgomo huo ndani ya siku saba iwapo mzozo hautatatuliwa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































